Nipe Nafasi || Isaac Ongere Anyolo

Kama wadhani amani ni Nafuu kuipata Jaribu Umwagaji damu.


WAHUSIKA

WAHUSIKA
OTENYO					:Kijana wake chifu na Moraa
ONWONG’A				:Chifu wa kabila la Kiborabu
CHEROTICHI				:Bintiye Mzee Salati kabila la kisotiki
KASISI					:
MORAA:					:Mamake Otenyo na bibiye Chifu ONWONG'A
WANAMUZIKI				:
MZEE SALATI				:Babake Cherotichi kiongozi wa kabila la kisotiki.
WAZEE					:Wale wa kiborabu na Kisotiki.
MLINZI MKUU				:Anayesimamia usalama wa kiborabu.
MZEE MKUU				:Anayesimamia baraza la wazee wa kisotiki.
WAPIGANAJI				:

WASIFU KUHUSU MWANDISHI

Mwandishi wa tamuthilia hii Nipe nafasi Isaac Anyolo Ongere ni Mzaliwa wa jimbo la Bungoma.Ni Muhitimu wa somo la Ununuzi kutoka chuo kikuu cha Mlima kenya.Shauku ya uandishi ilipiku taaluma yake.Ameandika Michezo ya kuigiza ambayo imeshinda mashindanoni za tamasha ya michezo ya kuigiza na filamu katika kitengo wizara ya elimu kwenye mashule.Pia ni mwandishi wa hadithi fupi na riwaya ya Son of The soil ambayo imechapishwa. 

INKISIRI

Otenyo ni Kijana kutoka kabila la Kiborabu ambaye anataka kumuoa Cherotichi Mchumba wake mrembo kupindukia wa kabila la kisotiki.Ndoa hii inanuia kuchangia pakubwa katika kuleta Amani,Umoja,Utangamano na Uiano kati ya hizi jamii mbili ambazo zimemwaga damu tangu jadi kwa sababu ya uadui mkuu wa kihistoria na uchochezi kutoka kwa viongozi wao.Babake Cherotichi kiongozi wa Kisotiki ana  chuki na kabila la Kiborabu inayochangia yeye kupinga  harusi kati ya Cherotichi binti yake na Otenyo wa kabila adui .Ubinafsi,usaliti,uchochezi  vyote hivi kushuhudiwa.Ni kipi kinatokea mbeleni?

DIBAJI

(Kuna Shangwe na nderemo katika himaya ya Chifu ONWONG'A Mkuu wa kabila la Kiborabu,Jukuani Waimbaji wa kitamaduni wanawatumbuiza wageni mashuhuri katika harusi ya kitamaduni kati ya Cherotichi binti wa Mzee Salati kabila la Kisotiki naye Otenyo Kijana wa chifu ONWONG'A.Sherehe zimepamba ,ngoma zikichezwa na pia kuna wenye wananengua dansi .Muda kidogo tunashuhudia Bwana harusi akisindikizwa na jamii yake huku wakiwa wamevalia Malebo ya kitamaduni .Anaelekezwa mahala maalumu alioandaliwa.

KUSANYIKO:      (Wanainuka na kushangilia kwa kipekekee}
KINA MAMA:      (Wanapiga vigelegele) Aliliee………. (Muda baadae anafwata Bi harusi na jamii yake wote wakiwa kwenye Malebo ya kitamaduni wanajongea mbele hadi walipoandaliwa kukaa)
KASISI:      Jamii za pande zote mbili Kati ya Bi na Bwana Harusi, ni dhahiri kuonekana kwa mwanga baada ya giza. Harusi hii ni faida kwa sisi sote,(Makofi yakipigwa}itamaliza uhasama kati ya kabila hizi zetu mbili na tutakua na ushirikiano utangamano.Wakwe uheshimiana Kama wanavyosema wazee.(Kusanyiko wakishangilia kwa shagwe nderemo,vigelegele na Vificho}Tangu kale historia katika jamii hizi mbili imekua ya chuki,Uchochezi unaochangia vita vya umwagaji mwingi wa damu.
SALATI:      (Kiamuka na uzushi}Harusi hii haitaendele.
KUSANYIKO:      Haitaendelea!
KASISI:      Mbona Kiongozi Salati?
ONWONG’A:      Kuna jambo limekusononesha Mzee mwezangu?
SALATI:      Harusi haifanyiki.
MORAA:      Si mahari tulilipa mkwe wetu.
SALATI:      Wewe mwanamke mshenzi, nyinyi hata kabila la kiborabu hamujafunza wanawake wenu adabu.
CHIFU:      Mbona kuleta aibu mbele ya wageni,Mzee mwezangu 									tusijiaibishe hii harusi ndoto ya wengi.
SALATI:      Oteni kabisaa, Binti wangu Mrembo sana hafai kuolewa 								na huyu kipofu.
CHEROTICHI		: Baba namupenda na roho yangu yote.
SALATI			: Nyamaza, Huwezi olewa na hawa adui zetu .
CHEROTICHI		: Baba ingawa kipofu lakini roho yangu imemupenda. Kipendacho roho dawa.
SALATI			: Harusi haitafanyika.
OTENYO	:(Kienda kupiga magoti kwa Babake Cherotichi) Niruhusu nimuoe chaguo wa moyo wangu binti wako.
SALATI			: Binti yangu hawezi olewa na kipofu.
OTENYO	: Baba binti yako mrembo na tunapendana sana kama shilingi kwa ya pili.Ingawa mimi ni kipofu lakini Yeye ndiye mboni ya macho yangu.
SALATI	:(Kicheka kicheko cha madharau) kipofu wewe ulijuaje binti yangu ni mrembo na hata macho hauna ,Nimesema harusi hii haifanyiki.
OTENYO			: Sikuzaliwa kipofu, lakini wewe ndiye chanzo.
KUSANYIKO		:(Kiwa na Mshutuko)Chanzo ?
CHEROTICHI		: Kipi kilitokea mpenzi?
KUSANYIKO		: Tueleze….
OTENYO	: Sikutaka iwe hivi,Lisilobudi hubidi,Siri hii ya mimi kua kipofu nimeificha kwa muda mrefu ili kusiwe na uhasama 	kati ya sisi jamii ya Kiborabu na hawa wenzetu wa jamii kisotiki.Yote haya yalitokea nikitafuta amani.Usiku huo  mchafu wenye vilio vilivyojawa na ghadhabu na hamaki naukumbuka kama jana.Mengi yalitupata……
(Mwisho wa utangulizi)




ONYESHO LA KWANZA
SEHEMU YA KWANZA
KISEGERA NYUMA
{Ni usiku wa manane moshi ukitokea kila mahali,Nyumba zikichomwa ,akina mama na wato wakipiga nduri za uchungu na majonzi.}
(KWA CHIFU WA KIBORABU)
CHIFU				: Uvamizi umefanyika pasipo sisi kujua.
MLINZI MKUU			: Chifu wacha baragumu ya kuashiria uvamizi umefanyika ipigwe.
CHIFU	: Haraka sana, kisha baraza la usalama liamurishwe kuja 	sasa hivi mkutanoni.Lazima tuvamie pia sisi.Ukiona meno ya simba usidhani anatabasu.Kuvuna asali ya nyuki kuna gharama yake.
MLINZI MKUU			:(Kipiga baragumu mara kumi kuashiria uvamizi}										Puuu….Puuu…Puuu…Puuuu…Puuu….Puuuu….Puuu..Puuu…Puuu…Puuu..
Pembe inapigwa mara kumi mfululizo kuashiria  adui amevamia)
VILIO				: Chachirie…ehhh….Chachire… 
Chiombe chio Omoborabu…
(They have been taken away the cattles of Omoborabu)
****Mwisho wa Onyesho la kwanza
Sehemu ya kwanza*******




ONYESHO LA KWANZA
SEHEMU YA PILI
MUPIGANAJI 	:(Baragumu ya kuonyesha kushinda vita inapigwa mara tatu}Puuu…Puuu…Puuu..
WAPIGANAJI			:(Wakishangilia kwa pamoja)Ole-yo hoo..
SALATI	: Sisi kama jamii ya kisotiki tuna wapiganaji walio na ujizi tosha kwa vita,zana zetu za vita Si mikuki,mishale,ngao na teo ni dhahiri tosha.Najua mlikua mumejipanga vya kutosha ndo maana mumerudi wote .Ngombe tumewaleta nyumbani.Jamii ya kiborabu haituwezi,Tumewamaliza natutawamaliza wakijaribu kutuvamia.Twendini kijijini tukasherehekea ushindi wetu.Wanakijiji wanangojea habari njema kaa hii.
MPIGANAJI			: Oleyo hoo..
WAPIGANAJI	: Oleyo hoo..(Wanaimba wakitika huku wakiwa wamemubeba Kiongozi wao Salati aliyekua 	amewangojea kwenye mto Mirio unaogawanyisha 	Kisotiki na Kiborabu)
**************Mwisho wa Onyesho la kwanza
Sehemu ya pili****




ONYESHO LA KWANZA
SEHEMU YA TATU
(Vilio vinaendelea huku baraza likipagwa, wapiganaji pia wanajianda kungoja maagizo kutoka kwa chifu wa kiborabu kiongozi wao,Vilio vya wanakijiji wa kiborabu vinasika bila kuisha)

ONWONG, A	:(Barazani wakiwa wameketi kitako,baraza la walinzi na Mwanae kiongozi)Hii kabila ya kisotiki wamevuka mipaka. 
MLINZI MKUU		: Dawa ya moto moto.
ONWONG'A	: Vita vianzishwe mara moja.Damu yao imwagige zaidi kuliko vile ya kaliba yetu ya kiborabu imemwagika.Mifugo wetu lazima warudi.
OTENYO			: Tutumie njia mbadala isiyo ya vita.
ONWONG’A	: Muoga wewe,Ukiuwa kwa upanga utakufa kwa upanga.Hakuna njia mubadala ila vita.
OTENYO			: Baba hatutakua tumetatua chochote.Amani muhimu 									kuliko kila kitu.
ONWONGA	: Adui anakutapikia mdomoni na wewe unamupapasa ati kwa ajili ya amani.Natoa amri ya vita dhidhi ya kabila la kisotiki. baragumu ipigwe mara moja,Zana za vita zotezitolewe.Mkipata Musotiki uwa kata kichwa chake na kitupwe 	mtu Mirio.
MLINZI MKUU		: Ndio kiongozi.(Mlinzi mkuuu kitaka kuipiga otenyo anamunyang’anya)
OTENYO			: Ngoja kwanza.
ONWONG’A		: Nini tena?
OTENYO	: Zana zote za kivita zikitoka si tutamaliza jamii yote ya Kiborabu hata watoto wadogo wasio na hatia.
ONWONG’A		: Hawakufikiria hivyo.Kumbuka wakiti wote mtoto wa nyoka ni nyoka.
OTENYO	: Baba mimi kama mshauri wa baraza la usalama tunachukua barabara hatari zaidi kwa hawa wenzetu.
ONWONG’A		: Sijali, nimetangaza vita.
OTENYO	: Mbona ujali na wanaoenda vita si vita si damu yako!Usiku wa leo tumepoza wanajamii wengi sana,Sikia bado vilio vya kina mama na watoto.Tuende vitani tena tupoteze wengine haitakua busara.
ONWONG’A	: Mkuu wa ulinzi vimia iyo kabila ya kisotiki,Mtoto siku zote hujua anaeza chezea matiti ya mamake lakini mapera ya babake nikama kutupa mawe kwa mzinga wa nyuki kisha kusimama kuona ni kipi kitafanyika.
OTENYO	: Hapana, itakua bora iwapo mtaenda kuwatembelea waadhiriwa ,wapewe makao waliochomewa nyumba zao,wafariji waliofiwa .Wahakikishie usala,amani na utulivu.Mimi nimejitolea kuenda kutafuta amani baina ya sisi na hao majirani wetu wa kisotiki.Nina imani kuwa mababu zetu watatembea nasi katika hii safari.
ONWONG’A		: Wewe mtoto wa kiongozi ni hatari
MKUU WA ULINZI:		Mzikize babako.
OTENYO	: Uongozi ni kujitolea kwa hali mali,Naenda kwa ajili yetu sote.Ni heri mtu mumoja afe na amani ipatikana kuliko kufa wengi na amini ikosekane.
ONWONG’A	: Nitakupa walinzi jamii ya kisotiki haiaminiki.Wewe	ndiye mridhi sina mwingine
OTENYO	: Hapana Kama mnaamini mimi ndiye mridhi halali naomba nafasi. Sitakaa chini niangalie mambo yakienda kombo .Naomba nafasi.Nitaleta amani,Ugaidi utakoma.
MKUU WA ULINZI		: Wewe kiongozi mtarajiwa unahitaji ulinzi .
OTENYO				: Nitaende kepekee yangu msiwe na shaka.
ONWONG’A			: Mwanangu lakini……
OTENYO				: Baba mwanao shujaaa nipe nafasi.
ONWONG’A	:(Kikubali shingo upande} Haya basi nakuruhusu.(Baraza linapiga makofi huku baragumu ya kusistiza vita ikipigwa mara nne na Mlinzi mkuu)
BARAZA	:(Tambiko la amani lafanywa aende salama)Safiri salama kiongozi wetu mtarajiwa.Mababu Wakutangulie.
OTENYO				: Naenda ,nitarudi msiwe na hofu.(Anaondoka chumbani)

******Mwisho wa Onyeso la kwanza
Sehemu ya tatu*******




ONYESHO LA PILI
UTANGULIZI
MORAA		: Kijana wangu (Kilio kikimutoka)Mbona kuchukua uamuzi kaa 	huo,Hatua 					umechukua ni hatari kwenye usalama wako. Jamii hii tunakuhitaji.
OTENYO	:(Kimupiga pambaja) Mama ulizaa shujaa atakaye komesha vita hivi vywa jadi bila silaa au umwagaji wa damu.
MORAA	: Kivipi? vita hivi hauviwezi ,hawa majirani ni watu wasio na utu.Ni wanyama .Vita ndio vinawafaa.
OTENYO	: Usitumie matamushi ya uchochezi. nipe nafasi naomba baraka yako.Nimeamua nitumie njia  bora isiyo ya vita .Nina imani mtafurahiia matunda pande zote mbili kuleta amani,utengamano na uiano.  
MORAA	: Huoni iyo hatari mwanangu,Sina mwingine ila wewe, mwanangu siko tayari kukupoteza,Nisikize Usiende wacha wapiganaji waende kama alivyotaka babako,Kiongozi wetu.
OTENYO	: Mama nataka watu wetu na hao majirani wa kisotiki tuishi kwa amani bila wasiwasi.Vita ,chuki na uchochezi vinaturudisha nyuma kimaendeleo. Mimi mwanao, kua na imani 	nami.
MORAA	:(Kimupa kibuyu cha maziwa)Nimekusikiza, wacha nikupe nafasi.Nenda salama mwanangu.(Kitokwa na machozi)
OTENYE	:(Akikichukua kibuyu) Asante mama kwa kunipa nafasi nitarudi salama.(Anaondoka huku akimwacha mamake kwenye hisia mseto}
*******Mwisho wa Onyesho pili
Utangulizi




ONYESHO LA PILI 
SEHEMU YA PILI
HIMAYA YA KISOTIKI
SALATI			: Binti Wangu mrembo.
CHEROTICHI		:Abee baba.
SALATI			:Nina habari njema.
CHEROTICHI		.Habari njema! ipi iyo.
SALATI			walikiona cha-mtema kuni.(Akicheka na kuvuta kiko chake)
CHEROTICHI		:Cha mtema kuni !
SALATI			:Ndio.
CHEROTICHI		:Nani hao?(Kiwekelea nyungu ya maji chini)
SALATI			:Kwani wewe hujui adui zetu.Sasa aliyeongoza kuvamia kabila la kiborabu ndiye atakaye kuoa.
CHEROTICHI		:Atakayenioa!
SALATI			:Ndio mwanangu.
CHEROTICHI		:Kwa misingi ipi?
SALATI			:Hakikisho kamili huyo atakupa ulinzi tosha.
CHEROTICHI		:Haitawezekana.
SALATI			: Haitawezekana!
CHEROTICHI	: Tena mumekosea sana kwa kitendo cha vita vya umwagaji damu .Huo ni uwoga wa hali ya juu.Wenzetu wamemwaga damu,Mali yao mumewanyang’anya ,Nyumba zao mlichoma.Huo sio ubinadamu ni unyama .Kumbuka wakiti wa baba la njaa,Jamii yetu ya kisotiki tukilimbilia kwao wakawa wakarimu kwa kuipatia  jamii yetu chakula chao wakipendacho ndizi .Sasa tuko na shibe sahani tuliyoikulia tumeipiga take baada ya kuikojolea.Nyinyi ni waharibifu na wezi inafaa mufungwe jela.Huo si uongozi ulio bora.
SALATI			: Imekua hivyo desturi yetu tangu jadi.
CHEROTICHI	: Kumepambazuka baba amuka ,Nyakati hizi sio kama zile.Utengamano ,umoja uiano ndio kitu bora.Natamani ile siku jamii  la kiborabu wakiowana  na jamii ya kisotiki,tuzae na hawa wenzetu tufanye biashara nao,tutangamane vizuri.Huo ndio uhusiano mwema.Sio watu kuisha kama wanyama.Haina faida.
SALATI			: Wewe hujui chochote niondokee.
CHEROTICHI	: Naeza kua sijui chochote lakini ukweli ni kaa mimba haifichiki.Mumekosa sana, hawa wenzetu wana hasira na chuki.Watavamia.Wewe una ufahamu jamii ya Kiborabu hapana mchezo wakitangaza vita,Wavuke mtu Mirio hakuna 	kitu kitasalia kwenye hii ardhi ya kisotiki.
SALATI			: Vita tutapigana jamii yetu sio dhaifu vile unadhania.
CHEROTICHI	: Sitangoja ubinafusi wenu uzae njaa.
SALATI		: Watoto wa siku hizi hamuna adabu kwa wazazi wenu.
CHEROTICHI	: Baba heshimu uheshimiwe.Kumbuka anayeuwa kwa mukuki hufa pia kwa  mukuki.Fahamu pia mukuki wa Ngurue kwa mwanadamu mchungu.Yatakapokukuta usiseme sikukuambia.
SALATI	: Wewe naona nikikuoza afadhali nipewe ng’ombe wewe uende kwa kina ng’ombe.Msichana siku hizi umekua mjinga.Hakuna siku na haijawai tokea musotiki kuwa rafiki 	na muborabu.
CHEROTICHI	:(Kijishika kiuno) Mimi Cherotichi binti wa Mzee Salati kiongozi wa kisotiki nitabadilisha taasubi na kasumba kati ya jamii hizi mbili.Nitatafuta amani na hawa wenzetu.
SALATI		: Ati unasema nini..?
CHEROTICHI	: Baba nipe nafasi nirekebishe penye umekosea.Mwanadamu si mukamilifu siku zote ,yeye hukose .Kuvunjika kwa mwiko si mwisho wa mapishi.
SALATI	: Wewe ni mwanamke.Wanawake waoga .Wao utegeme musaada kutoka kwa wazee wao.
CHEROTICHI	: Wanawake hao waoga ndio huza vijana shupavu.
SALATI	: Potelea mbali vita tutapigana na iyo kabila pumbavu ya kiborabu,Mifugo wao tutachuka,nyumba zao tutachoma,vijana wao tutawakataka  vipande fisi wa mwituni wawale.Tutawafanya watumwa wetu.Kiongozi wa kisotiki nimesema.Ayepinga maneno yangu hufa kwa mukuki.
CHEROTICHI	: Sikujua nina baba wa roho nyeusi hivi.Kiongozi mukatili kwenye hisitoria ya wasotiki.
SALATI		: Niondokee..Mpumbavu wewe….
CHEROTICHI	: Baba nipe nafasi nitengeneze barabara bora yenye uhusiano mwema.Kizazi kijacho kifurahie.Historia isituhukumu katili.
SALATI		: Niondokee ,Msimamo wangu sibadilishi.Toka….
******Mwisho wa Onyesho la PILI
Sehemu ya kwanza******
Two Rivers by Star Zahra (c) 2022
ONYESHO LA PILI 
SEHEMU YA PILI
(Sehemu tulivu kwenye mto Mirio,Wimbo wenye saitu nyororo unamufanya Otenyo kusongea karibu}
OTENYO		:(Kipiga makofi)Wau..wau…wau..Una sauti nyororo ya kumutoa nyoka pangoni.
CHEROTI		:Kweli nyoka mwenyewe katoka pangoni.
OTENYE	: Samahani.Msichana mrembo kama wewe unafanya nini pekeyako mto mirio hujui ni hatari kwanza kwako wewe jinsia ya kike.
CHEROTICHI	:Nikiuliza wewe nawe unafanya nini huku pekee yako.
OTENYO	: Mimi huja kupata utulivu iwapo nina mzongo wa mawazo.Ndege humu huimba nyimbo nzuri,Nao mutirirko wa maji hunipendeza.
CHEROTICHI	:Kwanza wewe si mwenyeji wa huku.
OTENYO		:Kweli.
CHEROTICHI	:Wewe ni jasusi basi kutoka kabila la kiborabu.
OTENYO		: Mimi si jasusi.
CHEROTICHI	: Wewe ni muborabu.
OTENYO	:Hujakosea kabisa.Mimi ni balozi Kutoka jamii ya kiborabu natafuta himaya ya Mzee Salati mkuu wa jamii ya kisotiki.
CHEROTICHI	:Hapana nitaamini aje maneno yako, wewe ni jasusi napiga nduru.
OTENYO		:Haina haja.Mimi naitwa Otenyo, jee wewe?(Kimupa mkono)
CHEROTICHI	:(Kimupa mkono pia)Mimi naitwa Cherotichi.
OTENYO	:(Anamwangalia ndani ya macho)Ama kweli sijawai ona 	msichana mrembo kama wewe .Nipe ruhusa nami nikuite wangu wa moyo.
CHEROTICHI	:(Kitabasamu) Wako wa moyo!
OTENYO		:Kibisaa..
CHEROTICHI	:Una mchezo.
OTENYO	: Mimi siwezi fanya matani na binti nyota kaa wewe. ukweli ni udhaifu wangu.Roho ikipenda imependa.
CHEROTICHI	:Ni kipi kimekuleta katika ardhi ya kisotiki?
OTENYO		:Waona wewe ndo jasisu.
CHEROTICHI	: Sidhani kaa ni shughuli za kiubalozi ndo 	zimekuleta huku .
OTENYO		: Umudhaniaye siye ndiye.
CHEROTICHI	: Wacha niwe na imani nawe,Karibu kwetu hakuna matata.
OTENYO	: Asanta nashukuru ,Wewe kweli binti mrembo sana .Urembo wako naeza linganisha tu na waridi la uwa.Ama kweli wengine walizaa lakini wewe ulizaliwa.
CHEROTICHI	: Ua pia lina wakati wake ,halivumi milele ,hunyauka.
OTENYO				: Nikweli lakini likituzwa vyema lina faida nyingi.
CHEROTICHI			: Kama zipi.
OTENYO				: Nyuki hutengenezea asali.
CHEROTICHI			: Wewe mcheshi kweli.Nujua utokako ni vilio kweli.
OTENYO				: Hali si hali lakini ndo maana nimekuja kuongea na 	nyinyi wenzetu.
CHEROTICHI			: Wazo zuri hilo itakua vyema sana.Hata mimi nina hayo matamanio.
OTENYO				: Wewe si binti wa kawaida ninapokutazama.
CHEROTICHI			: Mbona?
OTENYO				: Hadhi yako Ipo ,juu hata vile unavyoongea.
CHEROTICHI			:(Anatabasamu)Sikujua hilo.
OTENYO				: Ila kwa urembo huu wote una kasoro moja.
CHEROTICHI			:(Kijiangalia Makini)Kasoro ipi tena.
OTENYO				; Umekosa roho yangu kisha ukamiliki.
CHEROTICHI			: Roho yako ,nifanyie nini na nina yangu.
OTENYO	: Nimekupenda cherotichi.(Kimupigia magoti)Tuchumbiane nikufanye uwe wangu wa ubani ,nikuenziaye moyoni.
CHEROTICHI			:(Anacheka sana)Sisi maadui tangu hapo jadi.Haitawezekana.
OTENYE				: Upendo ni zaidi ya vyote,Nipe nafasi nikupende.
CHEROTICHI			: Siwezi kukupa nafasi.
OTENYO	: Nipe nafasi Cherotichi hutajutia .Nakuhaidi nikitoka hii kazi ya ubalozi mikakati dhabiti itafanywa tuchukuane.
CHEROTICHI			: Wewe unaufahamu waongea na nani?
OTENYO				: Najua naongea na binti mrembo wa kisotiki.
CHEROTICHI	: Basi uyo binti waongea naye ni mwanea mpendwa wa Salati kiongozi wa kisotiki.
OTENYO	: Basi kuna mwanga.Jamii mbili zitashikana pamoja na tutaishi kwa amani bila vita na balaa.
CHEROTICHI	: Leta amani mutihani utakua umeupita .Nitakupenda kupindukia.(Kimushika mkono na kumuamusha)Haya nitakuongoza kwa himaya ya kiongozi wa kisotiki.Yeye ni mubishi na mpenda vita sana.
******Mwisho wa Onyesho la pili
Sehemu ya pili*******



ONYESHO LA TATU
MLINZI		: Kiongozi Salati, Muborabu amaonekana kwenye mipaka ya kisotiki na binti yako.
SALATI		: Na aangamizwe mara moja, huenda akawa jasusi.
MLINZI		: Nisawa kiongozi Amri yako itatekelezwa.
SALATI 	: Na itekelezwe mara moja. Aliingiaje kwenye ardhi yetu. Ulinzi dhabiti unahitajika. Msizembee kazini. Mjue hao wajinga wa jamii ya kiborabu waeza vamia wakati wowote. Vitengo vya usalama uhakikishe viko macho. Wazee wa baraza waitwe maramoja.
MLINZI		: Ni sawa kiongozi(Anaondoka}
******Mwisho wa Onyesho la tatu}




ONYESHO LA TATU
SEHEMU YA KWANZA
(Wapiganaji wanawafumania Otenyo na Cherotichi, Wanamupiga hadi anazimia wakidhani amekufu wanatoroka, Cherotichi anapambana kumusaidia hadi anamufikisha kwao, anamweka Chumbani mwake na kujuuguza majeraha kutumia ujuzi aliotoa kwa nyanyake wa kutibu. Siku chache anapata uafueni lakini macho hayaoni)
OTENYO		: Kipi kilitokea?
CHEROTICHI	: Tulivamiwa lakini kwa bahati nzuri haukuuwawa nikakuleta humu chumbani kwangu nimekua nikikushughulikia hadi ulivyo sasa.
OTENYO		: Mbona humu ndani mna giza.
CHEROTICHI	: Giza kwani hauoni.
OTENYO		: Sioni chochote.
CHEROTICHI	: Labda ni madhara ya yale mauvimu pumuzika utakua shwari.
OTENYO		: Nimekua kipofu sioni kabisaa.
CHEROTICHI	:Hapana hujakua kipofu .Jipe nafasi ya kupumuzika macho yako yatarudi kama kawadi.
OTENYO		:Nisawa tuu,Sikujua binti wa kisotiki ana roho safi kama sura yake safi.
CHEROTICHI	: Pumuzika tafadhali. Kisha ukipoa nimepanga ukutane na babangu ili muweze kuzungumuza zaidi. Walio kuvamia ni walinzi wake na haikua vyema.Ilikua bahati tu bure wangekuuwa.Wao ni wanyama hawanga utu kabisa.
*************Mwisho wa Onyesho la tatu sehemu ya kwanza*****




ONYESHO LA TATU
SEHEMU YA PILI
SALATI	: Wewe ni mtundu sana, utaweza mukaribisha adui kwenye himaya yetu, Hujui atachukua siri zetu na kutuangamiza.
CHEROTICHI	: Wewe unaona ulifanya haki kweli, Kama singekua kumusaidia hangekua hai
SALATI	: Hata ni heri hangekua hai. Yeye ni jasusi anafaa amalizwe mara moja. Walinzi…. (Akiwaita)
CHEROTICHI	: Ukijaribu kumuguza kijana wa watu.
SALATI		: Usinitishe.
CHEROTICHI	: mimi nitajitoa uhai.
SALATI		: Unataka kukufia kijana wa watu amekupa nini.
CHEROTICHI	: Siwezi ishi na kiongozi mukatili kama wewe. Kijana huyu ni balaozi ametumwa kwako kuongelea jinzi kutakua 	na amani utangamano na uiano kati ya hizi jamii mbili. Huna budi ila kumusikiza.
SALATI		: Sina mda wa kuzikiza huo upuzi.
CHEROTICHI	: Wacha kiburi na majivuno.
SALATI	: Nachelewa mukutano wa baraza la wazee, sina mda wa kuongea naye. Mwambie arudi kwa ardhi ya kisotiki na awambie tuko tayari kwa vita sio mazungumuzo, Nyumba zao tutachoma, tutamwaga damu, mifugo tutachukua, mabinti na mama zao tutawafanya vibaraka wetu.
CHEROTICHI	: Baba wewe utabadilika lini?
SALATI		: Kukubali matakwa yao itaonekana mimi kua mudhaifu. Heri vita kuliko amani.
CHEROTICHI	: Hujui unalosema wewe. Barazana nitamuleta na atasikizwa.
SALATI		: Usijaribu kupimana nguvu nami, Mimi babako mzazi.
CHEROTICHI	: Baba nisikizishe usiwe mubishi sana. Kijana wa watu amekuja na habari njema. Ni faida kwa jamii. Tumupe nafasi aeleze kilicho muleta.
SALATI	: Nitakubali kumusikiza tu kwa ajili yako lakini msimamo wangu vita havitakoma kati ya jamii hizi mbili.
CHEROTICHI		: Utakua umefanya jambo la busara baba hutajutia	kwa lolote.
SALATI	: Nasubiriwa mukutanoni na baraza la wazee nitarudi tuongee mengi zaidi na huyo mgeni wako.
CHEROTICHI		: Nisawa baba.
*********Mwisho wa Onyesho la Tatu
SEHEMU YA PILI




ONYESHO LA NNE 
UTANGULIZI

MORAA		: Vipi chifu, habari zikoje kuhusu kijana wetu.
ONWONG’A	: Sijapata habari zozote kuhusu kijana wetu Otenyo, Lakini natumai alifika salama na labda ashaanza kuridi.
MORAA		: Wewe waona njia yake itazaa matunda kweli.
ONWONG’A	: Tumupe nafasi shujaa wetu.
MORAA		: Nina uwoga sana sijui mbona nahisi kina kitu hakiko shwari
ONWONG’A	: Hizo fikira zako usiwe na shaka kila kitu kitakua shwari kabisaa najua halitaharibika jambo.
MLINZI MKUU	: Kiongozi siku imekua ndefu sana na yenye kazi nyingi.
MORAA		: Wacha nikawaandalie uji, najua umechoka sana.
ONWONGA	: Vipi wanakijiji, natumai mumewashughulikia vilivyo.
MLINZI MKUU	: Kujikaza tuu, lakini najua tumejaribu kulingana na uwezo wetu kuweka mambo sawa ila tutafanya mazishi ya pamoja kwa wale walio uwawa. Mipango kabambe inaendelea na kamati andalizi inayoshughulika.
ONWONG’A	: Hawa kisotiki walitukosea sana. Isingekua mwanangu ningewamaliza wote. Wamejenga uadui na uhasama.
MLINZI MKU	: Kiongozi wao ndiye shida, Ana uchochezi.
ONWONG’A	: Lakini mimi nilishawasamea sina chuki nao.
MLINZI MKUU	: Wewe mukarimu ingekua babako. Yule kiongozi alikua fujo. Wanakistoki wangekiona cha mtema kuni.
(Wakiendelea na maongezi yao, Moraa analeta Uji na kuwapa. Mlinzi mkuu anashukuru na kuendelea kukunya uji)
ONWONG’A	: Hakikisha kila kitu kiko laini. Wajua hao tunaongoza ndio mali yetu na lazima kutunzwa kabisaa.
MLINZI MKUU	: Nimekusikikiza kwa makini kiongozi nitatenda matakwa yako.
*************Mwisho wa utangulizi
Onyesho la Nne”






ONYESHO LA NNE
SEHEMU YA PILI
(Kwenye himaya ya Kiongozi Salati wazee wa baraza wamekusanyika ili wafanye mazungumuza na Otenyo.Wana kiu ya kusikia ujumbe anao}
(Kisa anasindikizwa na Cherotichi kikaoni cha wazee)
SALATI		: Karibu utueleze kilichokuleta.
OTENYO	: Asante wakuu wangu. Nimekuja kwa amani. Mbwa habweki akiwa 	na mfupa mdomoni.
SALATI		: Usianze matusi.
CHEROTICHI	: Baba tulia.
OTENYO	: Nimekuja na ombi la amani, uhusiano mwema na utangamano (Wazee wananong,onezeana)
MZEE		:Karibu tumekupa sikio.
OTENYO	:Tangu kale jamii hizi zetu mbili zimekua adui wakubwa 	sana.Umwagaji wa damu umeshuhudiwa,Sote tumepoteza wapendwa wetu ,mali na mifugo.Amani imekosekana kabisa.Mimi ndiye murithi wa ardhi ya Kiborabu.
SALATI		:Haiwezekani.
CHEROTICHI	: Mbona hukunieleza..
OTENYO	: Sasa mumenifahamu nyote.Najua nilivamiwa sasa mimi ni kipofu lakini nishawasame na ni siri ibaki ivo.Mzee Salati Kiongozi wa kisotiki na Waheshimiwa wazee niruhusu niowe binti yenu Cherotichi.Amani itadumi milele kati ya hizi jamii zetu mbili.
SALATI		: Haitawezeka.Tangu lini Musotiki akaoleka kwa Muborabu?
MKUU WA BARAZA	: Kijana wetu umeongea vizuri sana. Wazo lako zuri sana, nina matamanio yangu kuwe na amani, umojauiano na utengamano.
MZEE	: Wewe kijana mdogo lakini una busara sana. Nimesikiza maongezi yako ni ya manufaa sana. Kiongozi salati mzee mwenzetu tumupe nafasi.
SALATI	: Mimi siwaamini hawa waborabu. Yaeza kua njama ya kutuangamiza tufikirie, mbeleni. Mbona kushawishika haraka.
MZEE			: Maneno ya kijana huya ya kweli hayana dosari hata kidogo.
OTENYO	: Nitawapa muda mujadili. Nimemupenda binti yenu nipe nafasi tuwe wamoja. Suluhu rahisi ya kumaliza uhasama milele.
MKUU WA BARAZA	: Nimeona ukweli wako, Mimi naunga iyo ndoa ya jamii mbili ya uongozi kuja na kua pamoja. Faida itakua pande sote mbili. Tutafanya biashara pamoja, Tutazaa pamoja, Tutafanya maendeleo pamoja. Zaidi ya hayo najua upendo utakua. Sisi kaa baraza la wazeee tumekupa nafasi. Ila tu babake Binti yetu ndiye atakayefanya uamuzi wa mwisho. Tuwe na azimio la umoja.
SALATI			: Mimi sina pingamizi, Pole kwa maovu niliyokutendea.
CHEROTICHI	: Alililii, Makubwa hayo. Hutakua kipofu tena mimi Macho yako (Wanasherehekea wote kwa furaha na makofi)
MKUU WA BARAZA	: Kikao hiki kimekua cha mafanikio. Tuweke mikakati ili harusu hii ya kisotiki na kiborabu najua itakua ya kufanya.
OTENYO	: Asante wakuu wangu kwa kunipa nafasi hamutajutia. (Anatoka huku akisindikizwa na Cherotichi)
OTENYO			: Naondoka mpenzi, nitarudi kukuchukua.
CHEROTICHI		: Uharakishi bure serikali itabadilishwa.
OTENYO	:Sitakawia,Nakupenda wewe wangu.(Wanakumbatiana kisha anamusindikiza hadi mto Mirio na kumupa walinzi}
CHEROTICHI		:Nenda salama mpenzi wangu.
OTENYO			:Nawe baki salama .
********Mwisho wa sehemu ya pili*********
MWISHO WA SEGERA NYUMA.
OTENYO		: Hayo ndiyo nilipitia lakini nilisamea ili tuwe na amani.
SALATI		: Wakwe naomba musamaha nisameheni.
KUSANYIKO	: Tumekusamehe lakini hatutasahau. (Pande zote mbili zikisalimiana na kubadilishana vitu kama vile ndizi na maziwa kuonyesha amani, utangamano na uiano}
KASISI	: Sasa hawa wawiwli ni bibi na bwana. Wanasotiki na wanaborabu ni mashemeji. (shangwe, nderemo, vifijo,Sherehe inaisha na denzi huku maharusi wakituzwa}

MWISHO

Isaac Ongere Anyolo
Latest posts by Isaac Ongere Anyolo (see all)